Sunday 17 December 2017

Huyu ndiye mwigizaji anayelipwa 'mshiko mrefu' Hollywood




Muigizaji Mark Wahlberg kutokea “Hollywood” nchini Marekani ametajwa na jarida la Forbes kama muigizaji anayelipwa pesa nyingi nchini Marekani kwa mwaka 2017, hii ni kutokana na kufanya movies nyingi, hivyo amefanikiwa kuingiza dola millioni 10 za kimarekani ambazo ni zaidi ya bilioni 22.5 za Kitanzania.

Mark Wahlberg amewahi pia kushiriki kwenye movies mbalimbali kama Pain and Gain, The departed, Boogie Nights na nyingine nyingi ambazo zinaendelea kufanya vizuri kimauzo sokoni hadi leo hii.

Mwigizaji huyu amejikita katika sekta mbalimbali ambazo zinamuingizia kipato ukiachilia kufanya kazi za uigizaji, Mark Wahlberg pia ni mfanyabiashara, producer, rapper na alishawahi kufanya kazi za uanamitindo nchini Marekani.

0 comments:

Post a Comment