Sunday 31 December 2017

Korea Kusini yakamata meli ya pili iliyohamisha mafuta kwa meli ya Korea Kaskazini


Mamlaka nchini Korea Kusini zinasema kuwa zimekamata meli ya pili inayokisiwakuhamisha bidhaa mafuta baharini kwenda kwa meli ya Korea Kaskazini na kukiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Meli hiyo yenye usajili wa Panama kwa jina Koti, inazuiwa kwenye bandari karibu na mji wa Pyeongtaek.
Ina wahudumu raia wa China na Burma. Siku ya Ijumaa Korea Kaskazini ilifichua kuwa ilikuwa imeshika meli yeny usajili wa Hong Kong kwa kuhamisha tani 600 za mafuta baharini kwenda kwa meli ya Korea Kaskazini.
Umoja wa Mataifa uliiwekea vikwazo Korea Kaskania kwa kuendelea kufanya majaribio ya silaha za nyuklia.

0 comments:

Post a Comment