Bodi ya (CUF) ambayo ipo chini ya
Mwenyekiti wa (CUF), anayeungwa mkono na Msajili wa Vyama Vya Siasa
nchini, Profesa Ibrahim Lipumba imepigwa marufuku kufanya shughuli
zozote zinazoihusu Taasisi ya CUF mpaka pale shauri la msingi
litakaposikilizwa.
Naibu
Mkurugenzi Uwenezi wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Maharagande
amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa leo Disemba 19, 2017 mbele ya Jaji
Wilfred Dyansobera katika Mahakamu Kuu Dar es Salaam ambapo Jaji
Dyansobera ameitaka bodi hiyo inayodaiwa kuwa ni bodi feki
kutojishughulisha na kazi zozote za taasisi ya CUF.
"Mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera ameipiga marufuku bodi feki ya Lipumba kufanya shughuli zozote zinazoihusu CUF mpaka pale shauri la msingi litakapomalizika. Awali Jaji aliyatupilia mbali maombi ya Wakili msomi Ngole ya kumuomba Jaji asisome maamuzi hayo kwa madai kuwa wanakusudia kukata rufaa juu ya maamuzi ya Jaji kukataa kujitoa kusikiliza mashauri ya CUF. Jaji amesema hakuna hoja za kisheria zinazoizuia mahakama kuacha kuendelea na shughuli ilizozipanga" alisema Maharagande
Mbali na hilo Naibu Mkurugenzi Uwenezi wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Maharagande amesema kuwa CUF ni taasisi imara yenye viongozi makini na kudai kuwa kwa ushindi huo ni wazi kuwa CUF mpya inazaliwa muda si mrefu sana.

0 comments:
Post a Comment