Thursday, 14 December 2017

Mkutano wa Nchi za kiislamu wautambua Yerusalemu


Mkutano wa nchi za kiislamu uliofanyika jana mjini Istanbul umetangaza kuitambua Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wa Palestina, ukijibu uamuzi wa Marekani ulioipendelea Israel.

Rasimu ya taarifa ya pamoja iliyotolewa na jumuiya ya nchi za kiislamu OIC, pia imezitaka nchi zote duniani kuitambua Palestina na sehemu ya Jerusalem Mashariki inayokaliwa kuwa mji wake mkuu.
Wakuu wa nchi waliohudhuria mkutano huo, wamesema uamuzi wa upande mmoja wa Rais Donald Trump wa Marekani kutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Palestina ni "batili" na wameulaani kwa "kauli kali".
Rais wa Palestina Bw Mahmoud Abbas amesema kwa sasa Marekani sio mpatanishi wa kweli wa amani.

0 comments:

Post a Comment