Thursday 17 May 2018

TI akamwatwa nyumbani akiwa amelewa.



Rapper TI amekamatwa leo asubuhi nnje ya geti la kuingilia katika makazi anayoishi katika mji wa Atlanta baada ya kugombana na walinzi waliomkatalia kupita akiwa hana funguo ya kupita katika mlango mkuu wa makazi anayoishi. 

 
TI alikamatwa saa 10 na nusu asubuhi huku akiwa amelewa na kujaribu kutumia umaarufu wake kupita mlangoni na kuwauliza walinzi "Don't you know who I am?" Lakini walinzi walikataa kumruhusu kupita.


Mwanasheria wa T.I., Steve Sadow, ametoa madai kuwa mteja wake alikuwa amekamatwa kimakosa "alikamatwa vibaya." Alisisitiza kusema kuwa mteja wake alikuwa ameenda kumuamsha mlinzi wa nyumbani kwake lakini alivyofika polisi walijua amelewa.

 
Sadow alisema T.I. alijitambua mwenyewe na alitaka kuingia, lakini walinzi walikataa. Rapa huyo aliwasiliana na mke wake Tameka "Tiny"  ambaye alithibitisha kuwa mumewe anapaswa kuruhusiwa.

0 comments:

Post a Comment