Sunday 31 December 2017

Vincent Kompany ametunukiwa shahada ya uzamili


Mwanasoka na beki wa Man City Vincent Kompany ametunukiwa shahada ya uzamili katika utawala wa Biashara (Masters of Business Adminstration) katika chuo cha Manchester ncchini Uingereza.
Kupitia ukurasa wake wa InstagramVincent ameonesha hisia yake juu ya kupata shahada hiyo aliyoipata.
"Sikufanya yote haya kwaajili ya kupata shahada, nimefurahi kumaliza,  safari haikuwa rahisi kabisa, nilifeli sana ila kujituma kumelipa, uwezo ulikuja baadae, haya ni mafanikio makubwa na heshima kwa marehemu mama yangu, namshukuru mke na watoto wangu kwa kunitia moyo,  nashukuru watu walionifundisha kozi yangu ya MBA katika chuo cha Manchester Business School, ushauri kwa wanamichezo wengine, usitegemee tu uwezo na afya yako, control maisha yako, jifunze zaidi kwenye maisha yako, uwe mwanamichezo uliokamilika zaidi"ameandika Kompany.

0 comments:

Post a Comment