Bavicha wasema Wema hakuwa mwanachama Chadema bali Alikuwa ni Shabiki Tu
Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana Patrick Ole Sosopi amesema hayo juzi baada ya
kutangazwa kurithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Patrobas Katambi
ambaye amehamia Chama Cha Mapinduzi mwezi uliopita.
“Wema
alikuwa shabiki wa Chadema na Chadema ina wafuasi wa namna mbalimbali.
Wapo tunaowafahamu na tusiowafahamu. Wema hakuwa chochote ndani ya
Chadema. Wema hakuwahi kufanya ‘movement’ yoyote. Msiwe mnasema amerudi,
kwani anatoka wapi?"- Ole Sosopi.
Aliongeza; “Wema
hakuwahi kupewa kadi yoyote ya Chadema. Alikuja kwa matatizo yake na
ameondoka kwa matatizo yake lakini hakuwa na sifa hata ya kuwa mjumbe wa
nyumba kumi. Wema ameondoka peke yake, wacha waondoke".
Ole
Sosopi aliyeteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha kuwa kiongozi
wake, alisema kwa sasa Chadema inapitia kipindi muhimu
kitakachoiimarisha.
Hata
hivyo Ole Sosopi aliongeza kwamba CHADEMA wameweka mipango katika
katiba kuhusiana na watu wanaohama wakitaka kurudi ndani ya chama hicho
hawatakubaliwa mpaka wafanyiwe uchunguzi wa kutosha kama dhamira yao ni
njema kwani wao si kama daladala ambalo unapanda, unashuka ili mradi uwe
na nauli.
0 comments:
Post a Comment