Monday 1 January 2018

Anthony Joshua amtolea uvivu Tyson Fury

 

Bondia Muingereza Anthony Joshua ambaye ni bingwa wa uzito wa juu duniani kwa sasa akishikilia mikanda mitatu mikubwa amesema hatoendelea kumheshimu bondia Tyson Fury licha ya mafanikio aliyowahi kuyapata.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye mahijoano maalum aliyofanya jana, akisisitiza amefikia uamuzi huo kutokana na kile alikiita kuwa ni dharau za wazi anazofanya Fury dhidi yake na kumvunjia heshma kila kukicha.
Fury ambaye ni mwingereza pia, mara kadhaa amekaririwa akibeza ushindi anaoupata Joshua na akitaka jamii iache kumpongeza kwani hajafikia viwango vya ubora.
Katika mahojiano hayo Joshua mwenye mikanda ya ubingwa wa WBA, IBO na IBF alizungumzia ujio wa pambano lake dhidi ya Joseph Parker litakalofanyika mwezi machi mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment