Roger Federer amefanikiwa kuweka
hai matumaini ya kutetea ubingwa wa mashindano ya Tennis ya Australia
baada ya kufuzu nusu fainali kwa kumfunga Thomas Berdych wa Jamhuri ya
Czech katika mechi iliyopigwa jana.
Federer alishinda kwa seti ya 3-0 yenye alama 7-6 6-3 na 6-4, na
kumfanya afuzu nusu fainali kwa mara ya 14 katika kipindi cha miaka 15.
Katika mchezo wa nusu fainali Federer atacheza na Hyeong Chung wa Korea Kusini, aliyefuzu baada ya kumfunga Tennys Sandgren wa Marekani.
Chung anakuwa mchezaji wa kwanza anayekamata nafasi za chini kwenye viwango vya ubora wa tennis duniani kufika nusu fainali katika kipindi cha miaka 14 iliyopita, na kwa kuwa na miaka 21 anakuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufuzu nusu fainali ya michuano mikubwa.

0 comments:
Post a Comment