Thursday 25 January 2018

Zimbabwe yakaribisha uwekezaji kutoka nchi za nje


Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye yuko ziarani nchini Uswisi kushiriki kwenye Mkutano wa Baraza la uchumi Duniani huko Davos, amekaribisha wawekezaji wa nchi za nje nchini Zimbabwe, ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Rais Mnangagwa amesisitiza kuwa Zimbabwe iko wazi kwa nchi za nje, na jukumu kuu kwa serikali ya nchi hiyo ni kufufua uchumi, na itazidi kupunguza vizuizi kwa wawekezaji kutoka nchi za nje.
Rais huyo amesisitiza kuwa Zimbabwe itaimarisha utawala kwa kufuata katiba, na kusema kuwa kwa mujibu wa sheria, uchaguzi mkuu unafanyika kila baada ya miaka mitano, na uchaguzi mkuu mpya utafanyika kabla ya mwezi Julai mwaka huu.
Rais Mnanangwa pia ameeleza matumaini yake kuwa uchaguzi utafanyika kwa uhuru, haki na na utakuwa wa kuaminika, bila kutokea vurugu.

0 comments:

Post a Comment