Saturday 13 January 2018

Maandamano makubwa yafanyika nchini Tunisia



Maandamano makubwa yameendelea kufanyika nchini Tunisia hapo jana na kusababisha vurugu za kimabavu.
Wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia imesema, vurugu zimesababisha kifo cha raia mmoja na askari zaidi 60 kujeruhiwa, magari zaidi 50 kuharibiwa, na watu wasiopungua 600 wamekamatwa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Khalifa Al-Shaibani, amesema, kuna vijana wengi miongoni mwa waandamanaji waliokamatwa ambao wanahusishwa na vitendo vya uporaji, wizi na uchomaji moto, ambavyo vilivuruga utaratibu wa jamii.
Habari zinasema, maandamano hayo yametokana na kuongezeka kwa gharama za maisha na sheria ya fedha ya mwaka 2018 iliyosababisha kuongezeka kwa bei ya bidhaa.

0 comments:

Post a Comment