Wednesday 24 January 2018

Mapambano juu ya ufisadi kuwa ajenda kuu kwenye mkutano wa AU


Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Workneh Gebeyehu amesema mapambano dhidi ya ufisadi yatakuwa ni ajenda kuu ya mkutano wa 30 wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa.
Mkutano wa 30 wa Umoja wa Afrika ulioanza jumatatu na kuendelea hadi jumatatu wiki ijayo katika makao makuu ya Afrika mjini Addis Ababa, kauli mibu yake ikiwa ni "kushinda mapambano dhidi ya ufisadi, njia endelevu ya mabadiliko ya Afrika".
Akizungumza na waandishi wa habari, Bw Gebeyehu amesema kiwango cha ufisadi na mapambano dhidi yake kwa sasa vimekuwa kigezo muhimu cha kupima uwezo wa kitaasisi na utawala bora wa nchi moja. Pia amsema kutokana na kuwa asilimia 70 ya waafrika zaidi ya bilioni moja ni vijana, mapambano dhidi ya ufisadi ni mustakbali wa nchi za Afrika.

0 comments:

Post a Comment