Timu ya Houston Rockets ikiogozwa
na nyota wake James Harden jana imefanikiwa kuifunga, timu ya Miami Heat
kwa pointi 99-90, zilizofanya timu hiyo ijitengenezee mazingira mazuri
ya kufuzu nusu fainali ya ligi hiyo ngazi ya kanda.
Licha ya jitihada za nyota wa kimataifa Hassan Whiteside aliyefunga
pointi 22 peke yake, na kuifanya timu hiyo iongoze kwenye robo ya kwanza
ya mchezo huo, Miami haikuweza kujinusuru na ushindi mwembamba wa
Houston ambayo ilinufaika na kazi nzuri ya James Harden aliyefunga 28
peke yake.
Asubuhi hii kwa majira ya Afrika mashariki kunafanyika mechi nyingine kubwa za NBA mabingwa wa mwaka 2014, San Antonio Spurs wanacheza na mabingwa wa mwaka 2016 Cleveland Cavaliers, lakini Golden State Warriors wako ugenini kucheza na New York Knicks.

0 comments:
Post a Comment