Tuesday 9 January 2018

Nusu Fainali kombe la Mapinduzi

 

Timu ya Yanga ya Tanzania  bara itakutana na URA ya Uganda katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi wakati Singida United itakuwa kibaruani kucheza na Azam FC, mechi ambazo zote zinatarjiwa kufanyika kesho jumatano katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Hii ni baada ya matokeo ya sare ya 1-1 baina ya Yanga na Singida United katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ulioamua mshindi wa kwanza na wa pili kwenye msimamo.
URA wanaingia kwenye mechi hiyo ikiwa ni baada ya kukamilisha mechi yao ya hatua ya makundi kwa kuifunga Simba ya Dar es Salaam kwa goli 1-0.

0 comments:

Post a Comment