Tuesday 30 January 2018

Odinga ajiapisha Urais Kenya uwanja wa Uhuru Park

Raila Odinga amefika katika uwanja wa Uhuru Park huku akiambatana na viogozi  kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.
Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.

Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika uwanja huo. Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.
Punde tu alipofika na 'kula kiapo' Raila Odinga ameondoka.

Awali Raila Odinga aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ' si mapinduzi ya serikali' bali ni kuonesha demokrasia na kupinga ukandamizwaji.

0 comments:

Post a Comment