Tuesday 30 January 2018

Odinga atarajiwa kuapishwa leo kama Rais Kenya



Hali ya sintofahamu imeendelea kutanda nchini Kenya leo Jumanne,hiyo ni tu baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Raila Odinga, kushikilia kuwa ataapishwa leo kama rais wa nchi hiyo.
Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) umesema hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi. Baada ya sherehe hizo kuahirishwa mwezi uliopita, muungano mkuu wa upinzani nchini humo-NASA, bado unaendelea na msimamo wake wa kuwaapisha viongozi wake Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama Rais na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kenya.

Idara ya Polisi nchini humo tayari imepiga marufuku shughulihiyo na kuwatahadharisha wote ambao wanapanga kushiriki.
 Hali ya mapema leo alfajiri
Mwanasheria Mkuu Prof Githu Muigai mwishoni mwa mwaka jana alisema mpango wa kumuapisha Bw Odinga ni sawa na uhaini wa kiwango cha juu.
Inakisiwa kuwa idadi kubwa ya wafuasi wa upinzani, wamesafiri usiku kucha kutoka maeneo ya mbali ili kufika Nairobi kwa sherehe hizo.
Agosti 2017, uchaguzi ulipofanyika, tume ya uchaguzi ilitangaza kwamba alikuwa ameshindwa na Rais Kenyatta.
Kiongozi huyo wa upinzani alipinga matokeo hayo Mahakama ya Juu na uchaguzi huo ukafutiliwa mbali na uchaguzi mpya kuandaliwa tarehe 26 Oktoba.

0 comments:

Post a Comment