Wednesday 17 January 2018

Umoja wa Mataifa waupongeza China

Umoja wa Mataifa wapongeza mchango wa China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza mchango wa China katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuitaka China iendelee kutoa mchango kusaidia kuongeza hamasa ya dunia katika suala hilo.
Bw. Guterres amesema ahadi zilizotolewa kwenye makubaliano ya Paris hazijatekelezwa kikamilifu, na ahadi hizo zenyewe hazitoshi kupunguza ongezeko la joto duniani katika karne hii kuwa nyuzi mbili kuliko kiwango cha kipindi kabla ya mapinduzi ya viwanda au hata chini ya nyuzi 1.5.

0 comments:

Post a Comment