Tuesday 13 February 2018

ALBERT EINSTEIN NA MAWAZO YA JOSE MOURINHO


Na Raphael Mwenda
               Mwanafalsafa wa kijerumani Albert Einstein katika kitabu chake cha "THE WORLD AS I SEE IT" (Dunia kama ninavyoiona) katika ukurasa wa 68 ameelezea maana ya kuchanganyikiwa akisema " INSANITY : doing the same thing over and over again and expecting different results" ( Kuchanganyikiwa : ni kufanya kitu kile kile tena na tena na kutegemea matokeo tofauti) ni maneno machache yenye maana nyingi sana katika maisha halisi ya binadamu. Huwezi kufaulu mtihani ikiwa hujasoma ama kumuelewa mwalimu pindi akifundisha hapa Einstein ametoa picha kwa binadamu yeyote anaependa maendeleo kutofanya kitu kile kile kinachomkwamisha kila akikifanya. Mtoto anaejifunza kutembea akipiga hatua moja na kuanguka atatambaa na kufuata egemeo ili anyanyuke na kujaribu kutembea akiwa ameshikiria kitu kwani ameshaelewa kutembea pekeake itamletea shida.
           José Mourinho ni kiburi mjeuri haswa anajiamini hapendi kushindwa na hatamani. Katika historia yake ya ukocha José anasifika kwa kutengeneza ukuta mgumu kufungika (mabeki ngangari) ndio itazame Fc Porto iliyochukua ubingwa pale Veltins-Arena nchini ujerumani kilikua kikosi cha kawaida kilichojaa wanaume wapambanaji hasa ukuta makini ulijengwa na Ricaldo Carvalho, Pedro Emmanuel, Ricardo Costa na nahodha Jorge Costa Alex Ferguson na mbinu zake alishindwa kuupasua ukuta huu hatiame Monaco wa Didier Deschamps nao walishindwa kutamba mbele yao kule ujerumani hatimae Fc Porto ikachukua ligi ya mabingwa. Ugumu wa ukuta ule ulimfanya Deco na wenzie wacheze kwa kujiamini na katika ubora wao
            Ni timu gani haikuvutiwa na Jose Mourinho? Lakini ni Chelsea waliopata bahati ya kumnyakua kwa falsafa zake zile zile hakuwaangusha nahodha John Terry kisiki hasa akamleta Ricardo Carvalho mwamba kweli kweli akamchukua Jose Bosingwa moto wa kuotea mbali achilia mbali Ashley Cole muingereza aliedumu upande wa kushoto kwa muongo mzima mbele yao alimuweka Claudio Makelele katika ubora wake katika benchi Obi Mikel katika kiwango chake cha dhahabu alikua akisubiri achilia mbali chuma Michael Essien. Kwanini Frank Lampard asifunge? Kwanini Deco asifanye vizuri kwanini Didier Drogba asiweke heshima kwa mabeki wa dunia hii,kwanini Chelsea isishinde michezo yake?
            Itazame Interlezionale Milan iliboresha ufalme wake pale Italy baada ya José kuchukua timu ile akitokea Chelsea Samuel Etoo aliwika zaidi Diego Milito alifunga anavyojisikia achilia mbali Wesley Sneijder katika ubora wake walikwenda kuchukua ubingwa wa Seria A pamoja na ligi ya mabingwa ulaya bila kusahau Escudetto walifanya yote haya Christian Chivu muargentina mwenye roho mbaya akiwa kashikiria mbavu ya kushoto huku upande wa kulia ukiwa umetekwa na mbrazili mwenye nywele za jeshi kichwani Lucio katika ubora wake usimsahau nahodha Javier Zanetti muitaliano kisiki hasa mbele yao walisimama Thiago Motta na Esteban Cambiasso katika ubora wao waliwafanya Etoo na wenzake kucheza kwa Uhuru mkubwa sana na kufanya chochote wanachokihitaji wakiamini nyuma yao kuna watu stahiki wa kufanya kazi nzuri na hakika walifanya kiufasaha.
             Pale Real Madrid kuna kisiki anaitwa Sergio Ramos mbabe hasa jeuri kwelikweli lakini usisahau José ndie kocha aliemtoa upande wa kulia na kumuweka katikati na akawa bora kama alivyo leo Christiano Ronaldo alifunga mpaka alikera achilia mbali Karim Benzema na Gonzola Higuain Melsut Ozil alipiga pasi mpaka kero usimsahau farasi Angel Di Maria hakuchoka kukimbia kila kona ya uwanja nyuma yao kulikua na Sami Khedira na Xabi Alonso katika ubora wao walikua wakiwalinda Ramos na mwenzie mnyama mmoja mwenye roho mbaya kuliko simba mwenye njaa aliitwa Pepe Alvaro Alberoa alikua bora pia Marcelo hakua akicheza kwani hana roho mbaya ile Jose anayoihitaji kule kushoto kulikua na mreno Fabio Coentrao walifanya kazi nzuri sana katika ulinzi Madrid iliwaka ikazima ufalme wa Barca pale Hispania ikatinga nusu fainali mfululizo ikavunja rekodi ya magoli mengi katika ligi achilia mbali pointi mia na kitu walitisha hasa.
                José alirudi Chelsea ambako alifanya vizuri pia lakini alipofutwa kazi alielekea Manchester United huko habari ni tofauti kabisa na hali ni mbaya. Jose alichukua timu isiyo na ubora isio na mabeki wale aina ya Zanetti isiyo na kiungo aina ya makelele isiyo na mshabuliaji aina ya Ronaldo achilia mbali chipukizi makini kama Alvaro Morata hapa alimleta Eric Bailly ili ampate Terry mpya akamleta Mikhtaryan walau Ozil wa Madrid awepo ndani yake akamleta Zlatan ili Drogba awepo ndani yake akamalizia kwa kumleta Paul Labile Pogba kwa bei ya kufuru akamsahau makelele akamsahau Chivu alifumba macho kwa Ivanovic akiamini Antonio Valencia atamudu kucheza kulia vyema. Msimu wake wa kwanza alishika nafasi ya sita katika ligi wakashinda ligi ndogo ya mabingwa achilia mbali kombe la EFL.
             Hatimae msimu ukaisha na Mourinho akamleta Matic kuja kuwa Khedira wake pale Old Trafford akamchukua Linderlof kuja kumuongezea nguvu Bailly na sasa amemuweka Sanchez kuja kuwa mfalme mpya achilia mbali Romelu Lukaku. José akasahau kuwa hajawahi kuchukua ubingwa akiwa kampanga Sneijder kama beki wa kulia ama Di Maria kama beki wa kushoto akasahau kuwa Zanetti akiwa majeruhi  basi kwa ubora ule ule Matterazi alicheza nafasi yake José akadanganyika na ushindi dhidi ya Westham wanaohaha kubaki ligi kuu akasahau matatizo ya Smalling hakuhofia ubora wa Jones.
             October 21 pale Kirklees Stadium nyumbani kwa Huddersfield aliwaweka Chris Smalling na Phil Jones katikati na Ashley Young kushoto timu ikafungwa magoli mepesi sana January 31 pale Wembley Jose akarudia kwenda uwanjani na walinzi wale wale wasio elewana japo wanaongea lugha moja timu ikapigwa goli jepesi sana kabla ya Jose kuja kujifunga goli LA wiki akampa Pogba majukumu mazito uwanjani timu ikacheza hovyo kupindukia hakuchoka siku kumi na moja mbele amerudia tena kitu kile kile pale St James Park mwisho wa yote timu ikafanyiwa dhihaka wakaupoteza ubingwa wa uingereza sidhani kama Nolito,Navas na Wissam Ben Yerder watashindwa kuupangua ukuta huu kama utapangwa hivyo tena kwenye ligi ya mabingwa ulaya.
                Mtamsema sana Paul Pogba mtamtukana sana Romelu Lukaku mtamkataa Alexis lakini si makosa yao bali ni makosa ya mfumo, mfumo wa Jose akiwa Porto Chelsea Interlezionale na Real Madrid ni ule ule tatizo umekosa watu sahihi katikati ya uwanja na katika ulinzi. Nemanja Matic (30) umri umemtupa mkono hawezi kukimbia kila wikiendi Achilia mbali Valencia (32) anaejikongoja huwezi kupata ubora halisi wa Pogba ukiwa na Smalling na Jones katika ulinzi bila kusahau Ashley Young. Katika mechi dhidi ya Everton pale Goodison park ama hakika nilimuona Paul Pogba Juventus ndani ya uzi wa Manchester United ndio Paul alicheza nafasi yake hasa huku nyuma yake kukiwa na Nemanja Matic pamoja na  Ander Herrera huku katika ulinzi Marcos Rojo Pogba hakuwa na kazi ya kukaba alicheza vizuri sana lakini kutoka hapo Jose hakumpanga tena kwa staili ile alirudi kumtumia tena Pogba kama kiungo wa kushambulia na kukaba.
               Sidhani kama Pep Guadiola hana hamu ya kubadili kikosi chake hapana lakini amekwishaona wazi Sane Aguero na Sterling ndio watu wake sahihi huku Silva Fernandinho na De Bruyne wakifanya kazi nyuma yao achana na ukuta wake ambao hauna maneno lakini Jose amekua akibadili timu kila leo kila mechi hana kikosi halisi cha kwanza leo Anthony Martial kacheza vizuri upande wa kushoto kesho utamkuta winga ya kulia leo Mata kacheza vizuri kesho utamkuta benchi achilia mbali Luke Shaw na Marcos Rojo.
                  Insanity (kuchanganyikiwa) Jose amechanganyikiwa mwenyewe katika nyumba yake ameshindwa kutumia vizuri rasilimali watu alionao pale Old Trafford. Habari mbaya tu kwa Manchester United ni kuwa kamwe hawawezi kuchukua ubingwa wakiwa na Ashley Young kama beki wa kushoto na Smalling na Jones kama mabeki wa kati achilia mbali Nemanja Matic kucheza game kumi mfululizo. Asanteh Einstein kwa kuliona hili la José mapema na upumzike kwa amani.

0 comments:

Post a Comment