Friday 19 January 2018

Palestina yautaka Umoja wa Ulaya usaidie mchakato wa amani kati yake na Israel



Katibu mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO Bw. Saeb Erekat ameutaka Umoja wa Ulaya uchukue jukumu la kuokoa mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel.
Akizungumza mjini Ramallah hapo jana, Bw. Erekat ameutaka Umoja huo uchukue hatua halisi na zenye ufanisi na kulinda kanuni za kimsingi za kutimiza amani kati ya Palestina na Israel. Amesema kanuni hizo ni pamoja na mpango wa nchi mbili na kuanzisha nchi huru ya Palestina kwa msingi wa mipaka iliyowekwa mwaka 1967, mji mkuu wake ukiwa ni Jerusalem Mashariki.
Pia ameutaka Umoja wa Ulaya utoe msaada ili kuziba pengo kubwa linalotokana na Marekani kupunguza msaada kwa Palestina na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA.

0 comments:

Post a Comment