Tuesday 24 July 2018

Trump, Hassan Rouhan wajibizana waziwazi



Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa Iran, Hassan Rouhani wamejibizana vikali na kutoa vitisho huku uhasama baina ya mataifa hayo mawili ukiongezeka

Rais Trump ameandika kupitia mtandao wa Twitter, kwa herufi kubwa, kwamba "Iran itapata madhara ambayo ni wachache sana wamewahi kukumbana nayo katika historia iwapo itaitishia Marekani."
.
Aidha, Rais Rouhani awali alikuwa amesema kwamba sera za uadui za Marekani dhidi ya Iran zitasababisha vita ambavyo vitakuwa "vita zaidi ya vita vingine vyote."
.
Ikumbukwe kuwa Mei mwaka huu, Marekani ilijitoa kwenye mkataba wa nyuklia na Iran ambao ulikuwa umehusisha Iran kusitisa shughuli zake za nyuklia ili iondolewe vikwazo vya kimataifa

Marekani sasa imeanza kuiwekea tena Iran vikwazo licha ya pingamizi kutoka kwa Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani wote ambao walikuwa wadau katika mkataba huo wa mwaka 2015

0 comments:

Post a Comment