Saturday 17 February 2018

Ethiopia yatangaza hali ya hatari

Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya hatari(State of Emergency) nchini humo ikiwa ni siku 1 toka ajiuzulu Waziri Mkuu wake, Hailemariam Desalegn
Vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo vinasema haijawekwa wazi ni kwa muda gani hali hiyo itachukua kuisha

Inadaiwa Baraza la Mawaziri lilikuwa linabishana sana kuamua kama hali hiyo ichukue muda wa miezi mitatu au sita
Mwaka 2015, Ethiopia ilitangaza hali ya hatari iliyodumu kwa muda wa miezi 10 baada ya mamia ya watu kufariki wakati wa maandamano ya kutaka demokrasia

0 comments:

Post a Comment