Rais John Pombe Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta wamewaagiza Mawaziri wao kumaliza tofauti ndogondogo za kibiashara baina ya Tanzania na Kenya
-
Marais hao wamesema wanataka kuona biashara inazidi kukua na bidhaa zinanunuliwa na kuuzwa bila vikwazo vyovyote baina ya nchi hizo
-
Wametoa maagizo hayo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Agustine Mahiga na Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi
-
Pia maagizo hayo yametolewa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma na Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kaskazini wa Kenya Peter Munya
0 comments:
Post a Comment