Wabunge katika mjadala uliofanyika Bungeni siku ya Jumatano walitumia muda wao mwingi kulalamikia na kujadili ukosefu wa karatasi za kutumia chooni(Toilet Paper) na maji katika vyoo vyao
Swala hili lilijadiliwa kwa pamoja na Wabunge wa Chama tawala na wale kutoka vyama vya upinzani
Mbunge John Mbadi, alisema kwamba swala hilo la choo ni tete mno huku mabomba pia yakikosa maji hivyo basi kuwa vigumu kwa wabunge kutekeleza wajibu muhimu wa kuwa wasafi
Naye Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed, huku akiishutumu Kamati ya maandalizi alimwambia Spika kuwa chai inayotolewa Bungeni hapo haina maziwa na inafanana na ile inayotolewa wakati wa matanga
Aidha, Wakenya wamtoa maoni yao na kuwataka wabunge wao kubeba karatasi zao za kutumia baada ya haja kubwa Bungeni iwapo wameghadhabishwa na ukosefu wa karatasi hizo Bungeni.
0 comments:
Post a Comment