Wednesday 7 February 2018

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kuondoka Liberia


Kikosi cha polisi wa kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Liberia kitaondoka nchini humo mwishoni mwa mwezi ujao.
Katika hafla ya kuwaaga askari polisi wa kikosi hicho iliyofanyika jana mjini Monrovia, mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Farid Zarif amewapongeza kwa juhudi zao katika miaka 14 waliyokuwepo nchini Liberia. Amesema juhudi zilizofanywa na tume hiyo ni sehemu muhimu ya kazi za Umoja wa Mataifa barani Afrika, na kwamba katika miaka 14, tume hiyo imelinda amani na utulivu pamoja na usalama wa wananchi wa Liberia.
Akihutubia hafla hiyo, Rais George Weah wa Liberia ametoa shukrani zake kwa msaada na mchango uliotolewa na askari hao. Pia rais Weah amekutana na kikosi cha tano cha kulinda amani cha China nchini Liberia, na kuishukuru China kwa mchango wake mkubwa katika kulinda amani na utulivu nchini Liberia.

0 comments:

Post a Comment