Wednesday 7 February 2018

Rais wa Afrika Kusini akanusha kumweka kikaangoni Makamu wake


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini jana amekanusha ripoti kuwa anataka kumfukuza kazi makamu wake Bw. Cyril Ramaphosa, na kusema ripoti hizo hazina msingi wowote.
Jumanne Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini SACP kilitoa taarifa ikisema wamepata habari kwamba rais Zuma anataka kumfuta kazi makamu wake. Pia chama hicho kimesema, rais Zuma anajaribu kutumia wapiganaji wa jadi wa kabila lake la Zulu, taarifa ambazo rais Zuma pia amezikana.

0 comments:

Post a Comment