Sunday 11 February 2018

Korea Kaskazini yamwalika rais wa Korea Kusini kufanya ziara nchini mwake

 

Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amemwalika rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kufanya ziara nchini mwake katika wakati unaofaa na mapema iwezekanavyo.
Msemaji wa Ikulu ya Korea Kusini Kim Eui-Kyeom amesema kuwa dada mdogo wa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini Kim Yo Jong alikabidhi barua ya Kim Jong Un kwa Moon, ikionesha nia ya Kim ya kuboresha uhusiano ndani ya Wakorea.
Mwaliko huo ulitolewa kwenye mkutano usio rasmi kati ya rais Moon na ujumbe wa Olimpiki wa Korea Kaskazini ukimjumuisha mdogo Kim ambaye anahudumu kama makamu wa kwanza wa mkurugenzi wa Kamati Kuu ya chama tawala cha Wafanyakazi nchini Korea Kaskazini.
Akijibu mwaliko huo, rais Moon ametoa mwito wa kuandaliwa mazingira ili kuifanikisha ziara hiyo.

0 comments:

Post a Comment