Wednesday, 21 February 2018

Madonna amtabiria mwanae kuwa Rais Malawi


Kila mzazi duniani hupenda kuona mtoto wake akiwa anafanikiwa kwani kufanikiwa kwa mtoto huletwa na mzazi mwenyewe au jitihada za mtoto
Nyota wa muziki wa pop nchini Marekani Madonna amesema kuwa mwanawe David Banda atakuwa rais wa Malawi siku zijazo katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa Twitter akimsifu mvulana huyo mwenye umri wa miaka 12.
Mwanamuziki huyo wa Marekani ana watoto sita ,wanne akiwa aliwahasili kutoka Malawi. Madonna amekuwa na uhusiano mbaya na mamlaka ya taifa hilo la kusini mashariki mwa Afrika.
Mwaka 2013 Malawi ilimshutumu Madonna kwa kutumia ushawishi wake kuwatishia maafisa wa serikali akisisitiza mchango wake kwa taifa hilo mbali na kutaka kupewa heshima.
Meneja wa Madonna aliishutumu serikali ya Malawi kwa kiuwa na chuki dhidi ya shirika la hisani la nyota huyo la Raising Malawi ambalo alilianzisha 2006 mwaka huohuo aliomuasili David.
David Banda ndio mkubwa kati ya watoto hao wanne. Uasili wake ulizua hisia kali miongoni mwa raia kwa kuwa sheria ya Malawi inawataka wazazi waliomchukua mtoto kuishi ndani ya taifa hilo mwaka mmoja kabla ya kuasili mtoto.

0 comments:

Post a Comment