Baada ya sare waliyopata Chelsea dhidi ya Barcelona basi Mkufunzi Antonio
Conte amesema kuwa Chelsea "itajaribu kufanya kitu cha kipekee'' na
kuitoa Barcelona katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya sare 1-1
katika awamu ya kwanza.
Willian aliiweka kifua mbele The Blues
lakini Lionel Messi alisawazisha dakika 15 kabla ya mechi kukamilika
baada ya makosa ya Andreas Christensen katika mechi ya kufuzu katika
robo fainali ya kombe hilo.Barcelona ambayo iko pointi saba mbele kileleni La Liga haikutekeleza mashambulizi yoyote makali hadi waliposawazisha.
''Tulikuwa tunakaribia kuwafunga," alisema mkufunzi huyo wa Chelsea. ''Tulifanya kosa moja, ni aibu na tumevunjwa moyo na matokeo''.
Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje ya eneo la hatari kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu kupitia shambulio alilotekeleza akiwa maguu 20.
Hatahivyo dakika 13 baadaye, Christensen alifanya makosa kwa kutoa pasi mbaya iliochukuliwa na Andres Iniesta aliyeshirikiana na Messi ambaye alifunga bao lake la kwanza la vilabu bingwa dhidi ya klabu hiyo ya London.
0 comments:
Post a Comment