Klabu ya Manchester City chini ya
kocha wake Pep Guardiola usiku wa jana imefanikiwa kutwaa taji lake la
kwanza msimu wa 2017/2018 dhidi ya Arsenal katika fainali ya kombe la
Carabao uliopigwa uwanja wa Wembley jijini London.
Man City imeshinda goli 3-0, magoli ambayo yamefungwa na Sergio
Aguero dakika ya 18, Vincent Kompany dakika ya 58 huku David Silva
akishindilia msumari wa moto kwa kufunga goli la tatu dakika ya 65.
0 comments:
Post a Comment