Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesifu makubaliano
yaliyofikiwa na vyama vyama vya CDU/CSU na SPD vya nchini Ujerumani juu
ya kuunda serikali ya mseto wakiyataja makubaliano hayo kuwa ni habari
njema kwa bara la Ulaya.
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker
ameyakaribisha makubaliano ya kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani
kati ya vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU na kile cha Social
Democratic SPD. Bwana Juncker amesema anaikaribisha hatua ya serikali
mpya ya Ujerumani kuhusiana na dhamira iliyonayo katika masuala ya sera
za Umoja wa Ulaya.Martin Selmayr mkuu wa watumishi kwenye ofisi ya Juncker, ameyapokea kwa furaha makubaliano hayo yaliyo kwenye mkataba wenye kurasa 170 utakaofanya kazi kwa miaka minne, mkataba huo mwanzoni mwake tu unaanza na sura inayosisitiza Ulaya yenye nguvu, pamoja na nukuu nyingi za mfumo wa Umoja wa Ulaya katika sekta zote.
Rais wa zamani wa Bunge la Ulaya Martin Schulz, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa chama cha Social Democratic (SPD) anayetarajiwa kuchua wadhfa wa Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani katika serikali mpya, amepongeza makubaliano hayo ya kuunda serikali yaliyofikiwa hapo jana Jumatano pamoja na kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Schulz amesema hiyo ina maana kwamba Ujerumani sasa itarejea kwenye jukumu lake kama kiongozi wa Umoja wa Ulaya.
Bwana Schulz amesema jambo muhimu ni kwamba serikali iko tayari kuongeza zaidi katika bajeti ya Umoja wa Ulaya. Amefahamisha kuwa mara nyingi amezungumza na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa njia ya simu na kwamba anataka kufanya kazi pamoja na Ufaransa ili kufanikisha kuwepo na "Ulaya iliyo bora zaidi na inayozingatia haki."
0 comments:
Post a Comment