Friday 9 February 2018

Mwenyekiti wa Kamati ya AU akanusha madai ya China kufanya ujasusi kwa AU


Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesema, madai kuwa China ilikuwa inafanya ujasusi kwa Umoja wa Afrika ni uvumi.
Bw. Faki amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi baada ya Mkutano wa 7 wa kimkakati kati ya China na Umoja wa Afrika mjini Beijing.
Bw. Faki amesema, uhusiano kati ya Umoja wa Afrika na China umekuwa hauyumbiki, na ripoti kama hizo haziwezi kuharibu uhusiano kati ya pande hizo mbili. Amesisitiza kuwa hivi sasa Afrika inataka kushirikiana zaidi na China ili kuwanufaisha zaidi watu wa Afrika, na uvumi kama huo hautakuwa na athari yoyote.

0 comments:

Post a Comment