Monday 12 February 2018

Mazoezi yakukimbia husaidia mwili wa binadamu


Watu wanaofanya mazoezi ya kukimbia na kutembea wana mambo mengi yanayofanana. Wote wanatumia njia mbalimbali kufikia malengo ya kuimarisha afya ya mwili.
Changamoto inajitokeza ni kwenye faida na hasara za mazoezi ya kukimbia au kutembea ambapo kila kundi lina hoja zake ambazo zinatofautiana na kundi lingine. .
Wakimbiaji wanafikiri kukimbia kunachoma mafuta haraka, kuongeza mzunguko wa damu na kumaliza haraka mazoezi. Watembeaji wanasema athari za viungo vya mwili ni ndogo, mapigo ya moyo huenda vizuri. .
Njia ya kuondoa utata kwa makundi yote mawili ni kuwaruhusu wataalamu wa mazoezi kushauri faida na watu gani ambao wanastahili kukimbia au kutembea kulingana na afya ya mtu. .
Mazoezi ya Kutembea
Kutembea kunaepusha madhara mbalimbali ikiwemo majeraha ya magoti, kiuno na nyonga.
Kukimbia kunatumia nguvu nyingi za kukanyaga ardhi na kusababisha msuguano kwenye mifupa na muunganiko wa mifupa kuliko mazoezi ya kutembea. .
Mazoezi ya Kukimbia
Haina mjadala kuwa kukimbia kunachoma zaidi mafuta ya mwili kuliko kutembea.  Daktari Patrick Suarez, Mtaalamu wa afya ya Mifupa ameliambia Jalida la POPSUGAR kuwa mafuta ya mwili yanachomwa mara mbili zaidi kwa wakimbiaji kuliko watembeaji kwasababu kiwango cha mapigo ya moyo huongezeka maradufu. .
UAMUZI
Ikiwa unafanya mazoezi ya kutembea au kukimbia unaweza kuendelea nayo ili kupata faida zilizoainishwa hapo juu. .
Kulingana na Jo-Ann Houston, Mkuu wa Mafunzo wa kampuni ya GYMGUYZ anasema jambo la muhimu ni kutambua na kufurahia faida za muda mfupi na muda mrefu za kila zoezi unalofanya.

0 comments:

Post a Comment