Monday 12 February 2018

Kahukumiwa miaka 27 jela baada ya kuwapa mimba wasichana watatu wa familia moja.



Kijana mmoja  kutoka mitaa ya Ohio, Arnold Perry (34) amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela baada ya kumpa ujauzito binti wa miaka 12 pamoja na dada zake mapacha wenye miaka 14.

Arnold alikua akiishi kwa ufadhili nyumbani kwa watoto hao na alichukuliwa kutoka mtaani na mama wa watoto waliopewa mimba kwa sababu alikua hana kazi ya kufanya wala sehemu ya kuishi.

Wasichana wote walipewa ujauzito mwaka 2015 na 2016 na mmoja ametoa mimba wengine walijifungua kwa sababu mimba zao zilishindikana kutolewa kwa sababu ya hatua waliyofikia
Baada ya kuhukumiwa Anord aliomba msamaha kwa mama wa watoto hao na kujutia kwa alichokifanya
"I know now what I did was wrong, I wish I could take it back." .
.

0 comments:

Post a Comment