Friday 2 February 2018

Mkurugenzi West Ham asimamishwa kazi kwa ubaguzi


West Ham imemsimamisha kazi mkurugenzi wa usajili wa wachezaji Tony Henry kuhusu madai kwamba klabu hiyo haitawasajili teza wachezaji zaidi wa Afrika.
Henry anadaiwa kutoa kauli kuwa kuwa wachezaji wa Afrika huzua fujo wasiposhirikishwa katika mechi.
Katika taarifa yake, West Ham imesema kuwa haitavumilia ubaguzi wa aina yoyote ule na hivyobasi imemchukulia hatua mkurugenzi huyo kutokana na hatari ya madai yake.
Chama cha soka nchini Uingereza FA kimesema kuwa kitachunguza rasmi suala hilo.

0 comments:

Post a Comment