Friday 2 February 2018

Waziri wa mambo ya Nje wa Uingereza apongeza hatua za China kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu



Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw Boris Johnson amepongeza uamuzi wa China kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu na kusema uamuzi huo una manufaa makubwa.
Akiongea na waandishi wa habari baada mkutano kuhusu utekelezaji wa China wa marufuku ya biashara ya pembe za ndovu ulioandaliwa na Shirika la kuhifadhi wanyamapori WWF, kundi la wabunge wa China na ubalozi wa China nchini Uingereza, Bw. Johnson amesema China imetoa pigo kubwa dhidi ya ujangili kwa kufunga soko la ndani la pembe za ndovu, na kufanya uamuzi unaowapa binadamu fursa ya kubadilisha mwelekeo wa kuteketezwa kwa Tembo barani Afrika.
Amesema Uingereza iko tayari kushirikiana na China kupambana na ujangili na kulinda wanyama adimu. Pia ametaka Uingereza na Umoja wa Ulaya kufuata uamuzi wa China kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu.

0 comments:

Post a Comment