Huko nchini Ufaransa, magoli matatu yaliyofungwa na Angel Di Maria yameiwezesha timu yake ya PSG kushinda 4-1 dhidi ya Sochaux na hatimaye kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Ufaransa, huku Goli lingine moja likifungwa na Edinson Cavani.
Lakini timu nyingine iliyofuzu kwa hatua ya nane bora ya
mashindano hayo kutokana na mateokeo ya mechi za jana ni Olimpique de
Marseille ambayo iliifunga timu ya daraja la kwanza ya Bourg-en-Bresse
kwa magoli 9-0.
0 comments:
Post a Comment