Wednesday 7 February 2018

ASANTE 'DANKE' KLOPP .


Na RAPHAEL MWENDA.
        Adolf Hitler baba wa taifa la Ujerumani alikua dikteta hasa alikua na roho ya chuma ,mbishi na mwenye kiu ya mafanikio, Adolf Hitler hakupenda kushindwa na hakuamini katika kushindwa sijatambua na wala sina uhakika alivyokufa alizikwa wapi lakini aliwaachia wajerumani kitu kimoja 'roho ngumu' na kuamini wanaweza kufanya chochote ulimwenguni pamoja na ukatili wake lakini alikua mpenda maendeleo Mungu amlaze mahala pema bwana huyu Adolf Hitler.
                  
   Kuanzia kizazi na vizazi vya wajerumani inaaminika wana roho ngumu sana ndio namtazama Jurgen Klopp pale Liverpool ni mfano rahisi tu wa asili ya wajerumani. Klopp hakubali kushindwa hatamani kushindwa anajiamini kupitiliza. Ndio anachofanya klopp pale Liverpool huenda ni Pep Guardiola pekee anaeweza kufanya lakini nae si kwa kiwango kile cha klopp kidogo muargentina Mauricio Pochettino anajaribu pale Tottenham.
      Jose Mourinho hawezi kutoa hela kwenda kumnunua Andre Robertson hata kama atakua anauzwa paun laki 5 kamwe José hawezi ,si José tu sidhani kama Pep anaweza sifikirii kama Antonio anaweza huenda Arsene Wenger lakini nae maji yamemfika shingoni siku hizi simtazami akiweza. Anachokufanya Klopp ni kutaka kuirudisha Liverpool ile ya kina John Andre Riise, Sammy Hypp, Jamie Carragher wakiongozwa na Steve G pale katikati ya dimba lakini wakati huu si Steve tena bali ni mjerumani mwingine mwenye roho mbaya anaitwa Emre Can.
      Siitazami Liverpool ya 2018/2019 katika jicho la kinyonge bali katika jicho la uoga ulojaa maswali mengi ndani yake. Msenegali kutoka RB Leipzig Naby Deco Keita atatua Anfield mwezi juni mwaka huu kujakuongeza nguvu katika kikosi cha Liverpool. Anakuja katika timu kipindi ambacho hakuna papa mkubwa zaidi katika kiungo cha Liverpool. Naby anaujua mpira anafunga anatoa pasi nzuri za mwisho anapiga mbali bila kusahau silaha kubwa ya Liverpool anakimbia kama hakuna kesho. Wiljnadum ni mchezaji mzuri lakini spidi yake ni tatizo katika aina ya uchezaji wa Liverpool
            Kwa kipindi kirefu baada ya kuondoka kwa akina Carragher akaja Martin Skertal na Daniel Agger wakatengeneza ukuta mgumu kweli kweli pale Anfield lakini toka waondoke walikuja Dejan Lovelen na Joel Matip ambao wamekua wakiruhusu mabao mepesi sana binafsi sikuona Klopp akilifurahia hili lakini alikaa kimya na kuendelea kuwaamini. Tukumbuke kuwa Klopp akiwa na Burrosia Dortmund alikua na ukuta wa chuma hasa Weidenfella katika ubora wake ameshikilia nguzo Lukasz Piszczek kavimba upande wa kulia Matts Hummels na Neven Subotic wamevimba katikati ya dimba huku Marcel Schmelzer akiwa upande wa kushoto ulikua ukuta haswa.
            January mwaka huu Klopp akakata kiu yake kwa kuvunja rekodi ya uhamisho kwa beki kwa kumnunua Virgil Van Dijk kutoka Southampton kwa paun 75 milioni japo hajaanza vizuri maisha yake ya soka pale Anfield lakini niamini hatokua huyu ifikapo agosti mwaka huu msimu mpya utakapoanza. Sina shaka na Klopp kabisa huyu jamaa ni jeuri na anajiamini kwa kile anachokifanya pale Liverpool sitoshangaa kumuona James milner akikaa benchi na nafasi yake kuchuliwa na Tomas Lemar kutoka Ac Monaco ndio Liverpool wanahela ya kumuuza Phillipe Countinho wanauwezo wa kumnunua yeyote yule kwa wakati huu japo si Sera ya Klopp kutumia hela nyingi katika kuboresha timu. Anaamini katika falsafa ya vijana lakini mpira wa sasa haupo hivyo si yeye tu hata Pep anaesujudu sana vijana ametumia zaidi ya paun milioni 200 kununua ukuta wake pale Etihad.
             Wajerumani husema  Danke Klopp (asanteh Klopp) kwa kuinamisha kichwa chini na kukubaliana na dunia ya sasa asanteh kwa kukubali na kuamini kuwa huwezi kushinda mataji ukiwa na Trent Arnold kama beki wako wa pembeni asanteh kwa kuamini kuwa Jordan Henderson si namba sita halali wa kumiliki dimba la Anfield. Asanteh nausubiri mwezi agosti kwa hamu kuu nikiamini utakuja na dawa halisi ya magonjwa sugu pale Anfield. Danke Klopp.

0 comments:

Post a Comment