Monday 12 February 2018

Serena Williams ashiriki mashindano ya kwanza

 

 Ushindi mara mbili katika mechi za mchezaji mmoja mmoja aliopata Venus Williams kwenye mchuano wa hatua ya robo fainali ya kimataifa kati ya Marekani na Uholanzi, umeisaidia timu ya taifa ya Marekani kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.

Venus aliwashinda Richel Hogenkamp na Arantxa Rus kwa mechi mfuatano zilizokuwa na matokeo ya mfuatano yenye alama 7-5, 6-1 na 6-1, 6-4.
Ushindi mwingine muhimu wa Marekani ulitokana na matokeo ya ushindi wa CoCo Vandeweghe aliyemfunga Richel Hogenkamp kwa 4-6, 7-6, 6-3.
Katika mechi za wachezaji wawili wawili ndipo Serena alipoungana na dada yake venus kuunda timu moja licha ya kuwa walipoteza kutokana na Serena kutokuwa imara bado.
Lakini kwa kufuzu hatua ya nusu fainali, mwezi Aprili Marekani watacheza na Ufaransa ambao nao wamefuzu baada ya kuishinda timu ya taifa ya Ubeligiji.

0 comments:

Post a Comment