Watu 14 walifariki Jumanne katika maporomo ya ardhi na kuvunjika kwa
majengo wakati wa tetemeko kubwa la ardhi katika eneo la ndani nchini
papua new guinea, polisi na mfanyakazi wa hospitali walisema jumanne
huku ripoti ambazo hazikuthibitishwa zikitaja idadi ya waliokufa kuwa
30.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, tetemeko hilo la kiwango
cha 7.5 kwa kipimo cha rikta lilipiga katika eneo hilo mapema jana na
kuharibu miundo mbinu ya madini na nishati na kupelekea kampuni ya
Exxonmobil kufunga kiwanda chake cha gesi ya asili LNG. Nchi hiyo ni
muuzaji mkubwa wa gesi.
"Majengo mawili yalianguka na maporomoko ya ardhi yalisababisha vifo vya watu katika eneo la mendi mji mkuu wa jimbo la Southern Highland," alisema muuguzi katika hospitali ya serikali ya mendi ambako miili ilipelekwa ili kuhifadhiwa.

0 comments:
Post a Comment