Mwanamuziki wa
kutoka nchini Marekani Rihanna akiwa anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini
Senegal,lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea, chombo
ch habari cha Jeune Afrique kimeripoti.
"Tumeukataa ufreemason na
mapenzi ya jinsia moja" , shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema,
wakimshutumu mwaimbaji huyo kwa kutumia ishara za mazo na kuwa mjumbe wa
chimbuko la Illuminati , lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu
ambao hudhibit masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya
shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia.Shutuma hizo zimefutiliwa mbali na wasanii waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma,
Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika nyadhifa yake ya balozi wa shirika la elimu 'Global Partnership Foundation'
Shirika hilo linamaadhui wa kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.
Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani akisema kuwa atahakikishia usalama washirika wote wa mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment