Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmiliki wa Pantoni ya MV
Nyehunge, Said Mohammed kwenye gati la Kirumba wakati aliposafiri na
chombo hicho kutoka jijini Mwanza kwenda Ukerewe Februari 18, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
***
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea vitendo vya uvuvi haramu wa kutumia sumu kali ndani ya ziwa Victoria kwa sababu vinaharibu soko la samaki.
***
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea vitendo vya uvuvi haramu wa kutumia sumu kali ndani ya ziwa Victoria kwa sababu vinaharibu soko la samaki.
Aliyasema
hayo jana jioni (Jumamosi, Februari 17, 2018) wakati akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Kisorya wilayani Bunda mkoani Mara.
Alisema
kitendo cha kuvua kwa kutumia sumu kinaharibu soko la samaki la ndani
na nje ya nchi kwa sababu sumu hiyo inabaki hivyo kumuathiri mlaji.
Waziri
Mkuu aliwaagiza Maofisa Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenda
kutoa elimu kwa wavuvi wa eneo hilo juu ya madhara ya zana haramu za
uvuvi.
Alisema
baadhi ya wavuvi wanavua kwa kutumia nyavu zilizopigwa marufuku, kokoro
pamoja na mabomu jambo ambalo haliwezi kuvumilika kwa sababu zana hizo
zinaharibu uhai wa viumbe hai ndani ya ziwa Victoria.
Pia,
Waziri Mkuu alisema Serikali tayari imeshaagiza nyavu zinazofaa kwa
ajili ya uvuvi endelevu kutoka nje ya nchi ambazo zitauzwa kwa wavuvi
mbalimbali.
Waziri
Mkuu alisema wavuvi wote wanatakiwa kufuata sheria ikiwemo kuwa na
leseni za uvuvi kwa vyombo vyao, hivyo alimuagiza Afisa Uvuvi afanye
ukaguzi.
Alisema
Serikali inafanya uhakiki wa vyombo na wavuvi wote ili kubaini nani
anavua wapi na kwa utaratibu upi. “Kamati ya Ulinzi na Usalama simamieni
suala hili.”
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bunda Bw. Amos Kusaja kuhakikisha gari la kuhudumia wagonjwa
la Kituo cha Afya cha Kasahunga linakuwa na mafuta wakati wote.
Alitoa
agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliodai
kuchangishwa fedha za mafuta ya gari hilo mara wagonjwa wao wanapopewa
rufaa kwenda katika hospitali ya wilaya.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 18, 2018.
0 comments:
Post a Comment