Sunday 18 February 2018

Wanajeshi wa Israel washambuliwa kwa bomu mpaakani Gaza


Wanajeshi wa Israel wamejeruhiwa wawili kati yao vibaya wakati wa mlipuko karibu na mpaka wa Israel na Ukanda wa Gaza.
Jeshi lilisema kuwa bendera ya palestina ilikuwa ikipepea eneo hilo, na wakati wanajeshi walikaribia wakakumbwa na mlipuko.
Israel iliendesha mashambulizi ya ndege katika vituo vya kundi la Hamas kujibu.
Katika kisa tofauti vijana wawili wa kipalestina waliuawa kwa risasi zilofyatuliwa kutoka kusini mwa Rafah nchini Israel.
wawili hao walikaribia mpaka kwa njia ambayo ilitiliwa shaka, kwa mujibu wa jeshi la Israel.
Israel na wanamgambo wa Hamas ambao wamethibiti ukanda wa Gaza walipigana vita mwaka 2014.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na mlipuko huo wa siku ya Jumamosi ambao ulitokea kusini mwa mji wa Khana Younis

0 comments:

Post a Comment