Thursday 15 February 2018

YAMETIMIA-Zuma ajiuzulu

 

Chama tawala nchini Africa kusini cha ANC, kimepokea tangazo la kujiuzulu kwa Jacob Zuma katika nafasi yake ya Urais.
Afisa mmoja mwandamizi wa chama hicho amesema hatua hiyo italeta utulivu wakati nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali, Ameongeza kusema kuwa ANC haisherehekei hatua hiyo, kutokana na kwamba Zuma amekitumikia chama hicho kwa miaka 60.
Awali kupitia televisheni Bwana Zuma alisema hakubaliani na mahitaji ya uongozi wa ANC kwamba anapaswa kujiuzulu, lakini amejiuzulu ili kuepusha ghasia ambazo zingechafua jina lake.
Makamu wa Rais wa Africa kusini Cyril Ramaphosa atapigiwa kura na wabunge kama mkuu wa nchi na baadaye kula kiapo ndani ya siku chache zijazo.

0 comments:

Post a Comment