Wednesday 21 March 2018

Mark Zuckerberg aitwa katika kamati ya Bunge Uingereza



 Kamati ya Bunge nchini Uingereza imemtaka Mkurugenzi wa Facebook, Mark Zuckerberg kufika mbele yake ili kujibu maswali kuhusu utumiaji usio halali wa taarifa kutoka katika mtandao

Kampuni ya Uingereza iitwayo Cambridge Analytica inatuhumiwa kutumia taarifa kutoka zaidi ya akaunti milioni 50 za Facebook kumsaidia Trump kupata ushindi mwaka 2016 ingawa imekataa tuhuma hizo.


Wakati hayo yakitokea, Bodi ya Kampuni hiyo ya uvunaji 'data' ambayo inatuhumiwa katika sakata hili, imemsimamisha kazi Mkurugenzi wake ili kupisha uchunguzi.

0 comments:

Post a Comment