Kampuni ya Johnson & Johnson imeamriwa na Baraza la Mahakama kulipa dola bilioni 4.7 (takribani Tsh. Trilioni 10.7) kama fidia na faini kwa wanawake 22 waliodai kuwa bidhaa za kampuni hiyo zimewasababishia saratani ya ovari
Katika kesi hiyo iliyodumu wiki 6, wanawake hao na familia zao wamesema kuwa wamepata saratani ya ovari baada ya kutumia poda ya Johnsons na baadhi ya bidhaa zake
Mawakili wa familia hizo wamedai kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatambua kuwa bidhaa yao ya poda ya talc ilikuwa na madini mabaya ya 'asbestos' tangu mwaka 1970 lakini ilikosa kuwaonya watumiaji kuhusu athari
Hata hivyo, Kampuni hiyo ilikana tuhuma hizo na walisisitiza kwamba bidhaa hizo hazileti saratani. Nakuongeza kuwa imesikitishwa sana na ina mpango wa kukata rufaa
Uamuzi huo unakuja wakati ambapo kampuni hiyo kubwa ya dawa ikipambana na kesi 9,000 zinazohusisha bidhaa yake maarufu ya poda
Aidha, Mtaalumu wa mambo ya Afya, James Gallagher amedai kuwa kumekuwa na wasiwasi kwa miaka kadhaa kwamba kutumia poda yenye madini ya talc au talcum, hasa kwenye viungo vya uzazi, inaweza kuongeza hatari ya saratani ya ovari lakini ushahidi haujakamilika
0 comments:
Post a Comment