Thursday 1 March 2018

Mwanafunzi auwawa na polisi Kenya


Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Meru nchini Kenya, Evans Njoroge ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi jana Februari 27, 2018 katika maanadamano chuoni hapo

Wanafunzi hao waliandamana wakishinikiza Chuo hicho kupunguza ada kwa kiasi cha shilingi 8,500 za Kenya ambazo ni sawa na Tsh 188,566 na kuboreshewa miundombinu chuoni hapo

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho baada ya vurugu walikimbia nje ya chuo na kwenda kujificha mashambani baada ya kuona gari la Polisi
Shuhuda mmoja alisema kuwa maaskari baada ya kuwakosa chuoni walienda uraiani kuwatafuta, alisema mtoto mmoja aliwaelekeza Polisi wanafunzi hao walipojificha

Hatahivyo aliongeza kwa kusema alisikia mlio wa bunduki na alipotoka alimkuta askari anabadilisha mavazi yake na kubakia na nguo za kiraia
Kwa upande wa mashuhuda wengine wamesema kuwa polisi huyo aliyemuua mwanafunzi anafahamika ni Afisa wa jeshi la polisi la kituo cha Nchiru.

0 comments:

Post a Comment