Baada ya jopo la madaktari wa
klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa na jopo la madaktari wa timu ya
taifa ya Brazil washirikiana kumfanyia uchunguzi wa kina mwanandinga
Neymar, leo wamefikia makubaliano ya kumfanyia upasuaji baada ya kuona
hakuna njia mbadala ya kutatua tatizo lake zaidi ya upasuaji.
Madaktari hao wamethibitisha kuwa Neymar amevunjika mfupa wa mguu wa
kulia karibu na enka siku ya jumapili dakika ya 77 ya mchezo dhidi ya
Marseille iliyomalizika kwa PSG kuibuka mshindi wa magoli 3-0. Upasuaji
huo utafanyika wiki hii nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment