Thursday 29 March 2018

UEFA KURUHUSU MFUMO MPYA W WACHEZAJI 12 WA AKIBA



Shirikisho la soka barani Ulaya(UEFA) limethibitisha kwamba timu zitaweza kuweka majina 12 ya wachezaji wa akiba kwenye mechi za fainali za Ligi ya Mabigwa, Ligi ya EUROPA na Super Cup. Kwa sasa idadi ni wachezaji 7.
 
Aidha, katika sheria hiyo mpya ambayo itaanza kutumika msimu ujao, timu zitaweza kufanya mabadiliko mara nne katika hatua ya mtoano ya michuano, huku badiliko hilo la nne likiruhusiwa iwapo mechi itafika dakika za nyongeza

Timu zitaruhusiwa kusajili wachezaji wapya 3 kwenye michuano hiyo baada ya hatua ya makundi kumalizika. Ikimaanisha mchezaji anaweza kuchezea timu moja wakati wa hatua ya makundi halafu akasajiliwa na timu nyingine na kuichezea katika hatua ya mtoano

Pia katika Klabu Bigwa mechi zake zote zitakuwa zinachezwa muda wa 8pm GMT (Kwa Tanzania: saa 4:00 usiku majira ya joto na saa 5:00 usiku majira ya baridi)

Katika michuano ya EUROPA hatua ya makundi mpaka 16 bora mechi zitakuwa zinaanza saa 5:55pm GMT na 8pm GMT(Kwa Tanzania; 1:55 usiku na 4:00 usiku majira ya joto, 2:55 na 5:00 majira ya baridi). Michezo ya robo, nusu na fainali itachezwa saa 8pm GMT

0 comments:

Post a Comment