Saturday 21 April 2018

Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora



 Serikali imetangaza kusitisha mara moja majaribio yote ya silaha za nyuklia na makombora

Maamuzi hayo yamefikiwa ili nchi hiyo ijikite kukuza uchumi na amani kwenye rasi ya Korea

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amesema nchi yake haihitaji tena kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu kwa sababu imekamilisha lengo lake la kutengeneza silaha za nyuklia

Ameongeza kuwa ili kuunda mazingira ya kimataifa yenye kufaa kwa uchumi wa nchi hiyo na hatua hiyo itawezesha mawasiliano ya karibu na mjadala pamoja na mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa

Tamko hili limekuja siku kadhaa kabla ya mkutano ulioandaliwa kati ya Kim na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na mkutano na rais wa Marekani, Donald Trump mwishoni mwa mwezi Mei au mwanzoni mwa Ju

0 comments:

Post a Comment