Wednesday 4 April 2018

Marekani, China zapingana kibiashara



Marekani imedai ushuru wa forodha uliowekwa na China katika bidhaa zake 128 ziingiazo China sio haki.

 Hatua hii ni kama kulipa kisasi kufuatia Marekani kupandisha ushuru wa bidhaa za chuma cha pua na bati

Marekani imesema ushuru wake ulilenga bidhaa za chuma cha pua na bati zinazoingizwa nchini Marekani ambazo ilizichukulia kama kitisho dhidi ya usalama wa taifa hilo

Aidha, China imesema sababu hiyo kuwa ni ukiukwaji wa miongozo ya shirika la kimataifa la biashara, WTO

China imesema wanataraji Marekani itaondoa hatua zinazokiuka kanuni za WTO haraka iwezekanavyo ili kurejesha mazingira bora ya kibiashara kwa bidhaa zinazotoka na kuingizwa kati ya Marekani na China

0 comments:

Post a Comment